Afisa wa dharura katika shirika la Muhuri kaunti ya Monbasa, Francis Auma amelaani vikali mauji ya mbunge wa Kasipul kaunti ya Homa Bay Ong’ondo Were, huku akitaka idara ya usalama kuharakisha uchunguzi dhidi ya kisa hicho.
Kulingana na Auma, kisa hicho kina dhihirisha usalama wa taifa hili hauko dhabiti na wakenya wako katika hatari ya kuhasiriwa na wakora wanaoendeleza visa vya mauaji ya kiholela.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Auma amesema kuwa idara ya usalama, inapaswa kuharakisha uchunguzi dhidi ya kisa hicho na kufahamisha wakenya chanzo cha mauaji hayo.
Aidha, amesisitiza haja ya wizara ya usalama kuwahakikishia wakenya usalama wao, jambo ambalo litawapatia uhuru wa kuendeleza kazi zao za kila siku.
Kauli yake inajiri baada ya watu wanne kukamatwa kwa madai ya kuhisika na mauaji yao, yaliyo shuhudiwa siku ya jumatano juma lililopita.

