MAAFISA SITA WA KWS WAFIKISHWA MAKAMANI KUFUATIA KISA CHA MVUVI MMOJA KUPOTEA MWEZI FEBRUARI MWAKA HUU 2025 KAUNTI YA NAKURU.

Huenda familia ya Brian Odhiambo, mvuvi aliyetoweka baada ya kukamtwa na maafisa wa polisi Kule Naivasha ikapata haki baada ya maafisa sita wa KWS kufikishwa mahakamani hii leo kule kaunti ya Nakuru.

Kwa mujibu wa wakili wa familia hiyo Abuya Mogendi, kwa sasa uchunguzi ambao umekuwa ukiendelezwa na maafisa wa DCI kuhusiana na kisa hicho, unawapatia matumaini ya kupata haki.

Briana aliripotiwa kutoweka mnamo tarehe 10 mwezi februari mwaka huu wa 2025 na familia yake imekuwa ikihainga katika kutafuta haki dhidi ya mpendwa wao, kwani bado hajapatikana hadi kufikia sasa.

Aidha familia ya Brian ikiongozwa na mkewe Alvy Okello, pamoja na mamake Elizabeth Aum, imesisitiza haja ya kupata haki dhidi ya mpendwa wao huku wakitoa wito wa maafisa wa KWS kutoachiliwa hadi kesi hiyo itakapo kamilika.