SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YASEMA ITALIPA MADENI YAKE KWA WATUMISHI WA UMMA.

Serikali ya kaunti ya Kilifi kwa mara nyingine imeahidi kulipa marupurupu ya wafanyakazi wake kaunti hii.

Katika kikao na waandishi wa habari, kaimu katibu wa serikali ya kaunti ya Kilifi, Catherine Kenga amedhibitisha kuchelewashwa kwa malipo hayo na kusema kuwa serikali ya kaunti hii, imeweka mikakati ya kulipa fedha hizo.

Catherine amesema kuwa tayari fedha zimepatikana ili kufanikisha shughuli za malipo hayo.

Vile vile amesema kuwa afisi yake kwa ushirikiano wa ile ya bodi ya uajiri wa umma katika kaunti ya KIlifi, itaanzisha upya shughuli za kuwapanga wafanyakazi wake, kwa mujibu wa taaluma waliozo somea na hata uzoefu walio nao.

Aidha, ameahidi kutatua changamoto za watumishi wa umma katika kaunti hii ya Kilifi, ili kuhakikisha kuwa wanafanyakazi katika mazingira bora kwenye jamii.…..