WANASIASA WALAUMIWA KWA MADAI YA KUFADHILI MAGENGE YA UHALIFU.

Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, sasa anasema wanasiasa ndio wanaofadhili magenge ya wahalifu, yanayoendelea kuhangaisha wananchi wa kaunti za Pwani.

Waziri Murkomen, ametishia kuwatia nguvuni wanasiasa wanaohusika na masuala ya kufadhili magenge ya kiuhalifu katika kaunti za Pwani na kitaifa.

Akizungumza kwenye kikao na viongozi wa kaunti ya Mombasa, pamoja na wakuu wa idara ya usalama eneo la Pwani, Murkomen amesema kuwa pia, wizara yake haitawapatia ulizi wanasiasa wanaofadhili makundi ya kiuhalifu.

Katika kikao na waandishi wa habari, Murkomen ameahidi kutatua suala la magenge ya kiuhalifu huku akipinga madai, ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, kuwa serikali ilifadhili vurugu zilizoshuhudiwa katika kanisa alikokuwa eneo la Kasarani siku ya jumapili.