MAAFISA WALIOKUWA WAKIHUDUMU KWENYE WIZARA YA AFYA WAMTETEA GACHAGWA DHIDI YA SAKATA YA NETI ZA KEMSA.

Aliyekuwa waziri wa afya Susan Nakhumicha, amemwondolea lawama aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, kwenye sakata ya ununuzi wa vyandarua vya mbu, akisema gachagua hakuchochea kwa namna yoyote utoaji wa zabuni hiyo ya shilingi bilioni 3.7.

Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge, ya masuala ya kigeni, ili kupigwa msasa kuhusu nafasi ya mwakilishi wa Kenya, katika shirika la un habitat Nairobi, Nakhumicha alieleza kwamba taifa hili, lilipoteza mamilioni ya fedha baada ya sakata hiyo kulipuka.

Nakhumicha, amesema kuwa alifahamu kuhusiana na madai hayo wakati Gachagwa, alipofikisha mbele ya bunge la kitaifa, ili kujitetea kutokana na kashfa zilizo ibuliwa dhidi yake.

Kwa upande wake aliyekuwa katibu wa afya Peter Tum, ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Congo, amesema kuwa zabuni hiyo, iliondolewa kwenye idara hiyo na kukabidhiwa afisi ya katibu mwingine.