Wakaazi wa kaunti ya Tana River wameonywa dhidi ya kuwa na dhana potofu kuhusiana na nafasi za ajira kwenye mashirika na taasisi za serikali kuu.
Kulingana na seneta wa kaunti hiyo Danson Buya Mungatana, kuna haja ya wale walio na masomo ya hali ya juu, kutuma maombi ya kupata kazi hizo pindi tu zitakapo tangazwa.
Akizungumza katika kaunti hiyo, Mungatana amesema kuwa zipo nafasi nyingi za ajira, ambazo zimetengewa watu wa jamii hiyo, kutokana na suala la wao kuwa mojawapo ya jamii zilizo na watu kidogo kitaifa.
Kauli yake imeungwa mkono na mmoja wa viongozi wa kuu, katika uongozi wa shirika linalo husika na masuala ya umeme na Kawi la KENGEN, Rehema Hassan, ambaye amewasisitiza kujitahidi katika kutuma maombi ya kazi hizo ili kuboresha maisha yao kwenye jamii.

