KANISA LA KIANGLIKANA LAWANYIMA WANASIASA FURSA YA KUHUTUBIA WAUMINI.

Kwa juma la pili sasa wanasiasa akiwemo aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, wamenyimwa fursa ya kuwahutubia waumini wa kanisa la kianglikana.

Hapo jana, walipofika kuhudhuria ibada ya kutawazwa kwa askofu mpya wa dayosisi ya kianglikana mlima kenya Magharibi Gerald Muriithi, Gachagwa ambaye alikuwa ameandamana na wandani wake, ambao ni pamoja na kinara wa chama cha PNP, Martha Karua walasalia kimya kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ibada.

Aidha, baadaye viongozi hao walihutubia wananchi inje ya nyumba ya ibada na kuwarai vijana kutokubali kutumika na wanasiasa nchini.

Askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana humu nchini Jakson Olesapit, akingumza kwenye ibada hiyo, alisisitiza kuwa mazungumzo kuhusiana na siasa za taifa hili, hayapaswi kufanywa ndani ya nyumba za ibada.

Sapit amewataka wanasiasa kuheshimu ibada na kuhakikisha kuwa wanazingatia suala la kudumisha amani na uuwino kati ya wakenya wote.