WIZARA YA USALAMA WA NDANI YA DHIBITISHA KUTUPILIWA MBALI KWA MALIPO YA WAKENYA KUPATA VITAMBULISHO.

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, amedhibitisha kutupiliwa mbali kwa ada za wakenya waliofikisha umri wa kupewa vitambulisho vya kitaifa.

Waziri Murkomen amesema kuwa wizara yake imeanza kutekeleza agizo hilo lililotolewa na rais William Ruto alipokuwa kwenye ziara yake katika kaunti ya Nairoibi wiki iliyopita.

Awali wakenya ambao wanatuma maombi ya kupata vitambulisho vya kitaifa walilazimika kulipa shilingi mia tatu ili kupewa huduma hizo katika afisi husika kote nchini.

Aidha Waziri Murkomen amesema kuwa idadi kubwa ya wakenya wamekosa kutuma maombi ya kupata stakabadhi hiyo muhimu kutokana na hali ngumu za kiuchumi wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule za upili na baadhi ya wale waliomaliza kidato cha nne mwaka 2024.