WANAFUNZI WA CHUO CHA BANDARI KAUNTI YA MOMBASA WAANDAMANA.

Wanafunzi wa chuo cha mafunzo ya masuala ya ubaharia kaunti ya Mombasa, wamefanya maandamano kupinga utendakazi duni wa usimamizi wa shule hiyo.

Kulingana na wanafunzi hao, baadhi ya wahadhiri katika taasisi hiyo wamekuwa wakisusia shughuli za kuwafunza kwa madai ya kutolipwa mishahara hao.

Wakiongozwa na Dancan Odongo na Salim Tsuma, wamesema kuwa watakuwa wakiandamana kila jumatatu, hadi pale matakwa yao yatakapo angaziwa kiukamilifu na serikali kuu ama usimamizi wa taasisi hiyo.

Vile vile wamesema, tangia walipo jiunga na taasisi hiyo, hawajakuwa wakipewa matokeo ya mtihani ambayo wamekuwa wakifanya.