Rais William Ruto amepongeza hatua ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi wa mwaka 2022 Raila Odinga, kuunga mkono utendakazi wake katika taifa hili.
Kulingana na Rais, hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kupiga vita visa vya ukabila na ubaguzi wa wakenya wa maeneo mbali mbali ya taifa hili, hasa katika masuala ya maendeleo na siasa.
Akihutubia wakenya katika majengo ya jumba la mikutano la KICC kule Jijini Nairobi, baada ya kutia sahihi mkataba wa makubaliano na Odinga, Rais Ruto ameonekana kuwa mwenye furaha zaidi na kuelezea kuwa na imani ya kusaidiwa na Raila, katika kutatua changamoto za wakenya.
Kwa upande wake Raila Odinga, amesema kuwa mkataba huyo unalenga kuchangia pakubwa kuleta amani kati ya wakenya na hata kutatua changamoto zao huku akiahidi, kushirikiana na rais Ruto ili kufanikisha ajenda za maendeleo.

