RAILA ODINGA KASHIFU VISA VYA UTEKAJINYARA WA VIJANA NCHINI.

Aliyekuwa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameitaka serikali kukomesha visa vya utekajinyara wa vijana wa taifa hili.

Akizungumza hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Odinga amesema kuwa mauaji ya vijana wa taifa hili, siku chache baada yao kutekwanyara ni ukiukaji wa haki za kibinadam na sharti serikali itoe agizo la kusitishwa kwa visa hivyo.

Waziri mkuu huyo wa zamani, amesisitiza kuwa bado viongozi wa chama cha ODM, wataendelea kupinga kuendelezwa kwa visa hivyo katika taifa hili hadi pale vitapo komweshwa.

Kauli yake imeungwa mkono na gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro, ambaye pia amesema kuwa kama viongozi wa chama cha ODM wanaimani na maamuzi ya Raila Odinga na wataendelea kuunga mkono muelekeo wa kisiasa atakao toa.