VIONGOZI WA KIDINI WAONYWA DHIDI YA KUTUMIKA KISIASA ILI KUPINGA SERIKALI KUU.

Naibu kinara wa walio wengi kwenye bunge la kitaifa Owen Yaa Baya amewaonya viongozi wa kidini, dhidi ya kutumika kisiasa ili kukosoa serikali ya kitaifa.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye pia ni mbunge wa Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi, licha ya viongozi wa kidini kuwa na haki ya kukosoa serikali, wanapaswa kutekeleza wajibu huo kwa kuzingatia ukweli, haki na usawa.

Akizungumza na lulu fm, Owen amesema kuwa hatua hiyo, itasaidia katika kuhakikisha kwa wakenya hawapotoshwi na kauli za viongozi wa kidini, wanaokosoa utendakazi wa serikali na hata kusishuhudiwe tofauti za aina yeyote, kati ya viongozi serikalini na wale wa kidini.

Kwa upande wake askofu mkuu wa kanisa la kianglikana jimbo la Malindi, Ruben Shukuru Katite amewaonya viongozi wa kidini, dhidi ya kukosoa serikali pasi na kuwa na ufahamu wa kina, kuhusiana na kile wanacho zungumza.