Zaidi ya asilimia 23 ya ndoa elfu 15 za waumini wa dini ya kiislamu, zinazo fungishwa katika afisi ya Kadhi hapa nchini kenya, zimekuwa zikiishia kuvunjia na wanandoa kupeana talaka.
Haya wa mujibu wa kadhi mkuu nchini Kenya, Shehe Athman Hussein Abdhulhalim, ambaye ameelezea kuwa na wasiwasi wa maisha ya kizazi cha siku za uosoni.
Hussein amewaonya wanajamii dhidi ya kuendeleza maisha ya ndoa, pasi na kufuata sheria na misingi ya dini, kwani ni mojawapo ya masuala ambayo anadai yamechangia katika kushuhudiwa kwa visa vya talaka.
Wakati uo huo Kadhi huyo amesema kuwa, idadi kubwa ya vijana katika dini hiyo, wamekuwa wakilalamikia gharama za juu zaidi wakati wanapotaka kufunga ndoa.

