Rais William Ruto amewasuta baadhi ya wapinzani wake wa kisiasa kwa madai ya kuendeleza mipango ya kuhakikisha kuwa, hapati uungwaji mkono kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Kwa mujibu wa rais, viongozi hao wamekuwa wakiendeleza siasa za ukabila kinyume na jinsi ambavyo, serikali ya Kenya kwanza imekuwa ikijitahidi kuunganishwa viongozi wa mirengo tofauti katika taifa hili.
Akihutubia umma katika eneo la Ndau kaunti ya Lamu, rais amewataka wapinzani wake, kuendeleza siasa za maendeleo na umoja kwa wakenya.
Vile vile amewaonya wakaazi wa kaunti ya Lamu dhidi ya kuganywa na baadhi ya wapinzani wake, kwa misingi ya dini na ukabila na badala yake kuawasisitiza kuungana, ili kufanikisha ajenda za maendeleo kaunti hiyo.
Kwa upande wake gavana wa kaunti hiyo Issa Timamy, amempongeza rais Ruto kwa kuondoa kigezo cha jamii za eneo hilo, kupigwa msasa wakati wanapotafuta vitambulisho vya kitaifa.

