WANANCHI ENEO LA GARSENI KAUNTI YA TANA RIVER WANUFAIKA NA MPANGO WA HUDUMA MASHINANI.

Jumla ya wananchi 300 katika eneo la Mnazini eneo bunge la Garseni kaunti ya Tana River, wamenufaika na mpango wa huduma mashinani unaoendelezwa na maafisa wa kituo cha Huduma Center kaunti hiyo.

Afisa mkuu wa kituo hicho eneo la Hola kaunti hiyo Jackson letangule amesema kuwa wananchi hao wamenufaika na huduma kama vile usajili wa vyeti muhimu vya serikali ambavyo ni pamoja na vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa.

Akizungumza na wanahabari, amesema kuwa idadi kubwa ya wananchi wa wa eneo hilo bado wanauhitaji mkubwa wa huduma hizo na hivyo kuna haja ya kuwepo kwa mipango wa zoezi hilo kufanyika mara kwa mara.

Letangule amesema kuwa wananchi wengi wamepoteza stakabadhi hizo muhimu baada yao kuathirika na mafuriko mwaka jana na hata wengi wao kulazimika kuhama makaazi yao.