SERIKALI YA KITAIFA YATAKIWA KUPUNGUZA IDADI YA KAMPUNI ZA VILEO.

Naibu mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Mutahi kahiga, ameitaka serikali kuu kupunguza kampuni zilizoidhinishwa kutengeza vileo nchini, ili kuzipiga jeki juhudi za serikali za kaunti, kupambana unywaji wa pombe haramu.

Kwa mujibu wa Kahiga, ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Nyeri, kumekuwa na ongezeko la idadi ya kampuni zinazouza pombe, licha yake kutoidhinishwa na halmashauri ya kukagua ubora wa bidhaa nchini KEBS.

Kahiga vile vile amesema kuwa kupunguzwa kwa idadi ya kampuni hizo, kutasaidia pakubwa katika kukabiliana na suala vijana, kuathirika kiafa na hata wengine kupotea uhai, kufuatia suala la wao kubugia pombe kupita kiasi.

Vile vile amedhibitisha kuwepo kwa mikakati ya kaunti ya Nyeri pamoja na muungano wa kaunti za mlima Kenya, kukabiliana na utumizi wa pombe, juhudi ambazo zilikuwa zimeanzishwa na aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa.