MWANAHABARI LEONARD MAMBO MBOTE AAGA DUNIA.

Mwanahabari mkongwe Leonard Mambo Mbotela ameaga dunia.

Binti yake Anne Mbotela amethibitisha kifo chake.

Mwanahabari huyo mkongwe amekuwa akiugua kwa muda na ameaga mwendo wa saa 9:30 asubuhi leo Ijumaa.

Mbotela ni mumewe Alice Mwikali, na kwa pamoja walipata watoto watatu Aida Mbotela, Jimmy Mbotela na George Mbotela.

Mwanahabari huyo mahiri alisifika kwa kipindi chake maarufu cha Jee Huuu ni Ungwana, kilichopeperushwa kwenye redio na runinga ya KBC.

Kipindi hicho kilianza mnamo mwaka 1966.

Aidha, mbotela alizaliwa katika eneo la FreaTown kaunti ya Mombasa, mwaka 1940, akiwa kifungua mimba wa James na Aida Mbotela.

Kutoka kituo cha habari cha Lulu fm tunasema Makiwa kwa familia.