Mbunge wa Rabai kaunti ya Kilifi, Kenga Mupe amewataka vijana katika eneo lake kukumbatia taaluma za mafunzo ya ubaharia, ili kunufaika na nafasi za ajira kwenye meli kimataifa.
Kiongozi huyo ameahidi kuunga mkono vijana hao, kwa kuwasaidia katika kutafuta nafasi hizo za ajira, ili waweze kujiendeleza katika maisha.
Akihutubia jamii katika eneo hilo Mupe, amewataka vijana wa eneo hilo kushirikiana na afisi yake, ili kufanikisha suala la wao kupata nafasi hizo za ajira.
Wakati uo huo Mupe, ameahidi kuwa afisi ya hazina ya NG-CDF katika eneo bunge hilo, itawapatia ufadhili wa shilingi elfu kumi na tano, vijana watakao jiunga na taasisi ya kwa mafunzo ya ubaharia.

