Wizara ya fedha inchini imesema kuwa tayari imetuma fedha zote zinazo hitajika, kufadhili shughuli za masomo kwa muhula wa kwanza katika shule za msingi za umma kote nchini.
Kulingana na waziri wa fedha John Mbadi, shule za msingi zimepokea shilingi bilioni 4.6 huku taasisi za JSS zikipokea shilingi bilioni 15.1.
Mbadi amewekawazi kuwa shule za upili, zimepokea shilingi bilioni 14, ambazo ni nusu ya kiasi hitajika cha shilingi bilioni 28.
Aidha, amesema kuwa wizara yake inaendeleza ukaguzi wa ripoti ya madeni, iliyo wasilishwa kwake na kamati husika.

