Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Kenza Ondiek ameutaka muungano wa wahandisi nchini, kukoma kupinga uteuzi wa Aisha Jumwa, kuwa mwenyekiti wa bodi ya barabara, kwa madai ya kutokuwa na tajiriba hitajika.
Kulingana na Ondiek, uteuzi wa Jumwa ni njia mojawapo ya serikali ya Kenya kwanza, kumpongeza kwa juhudi zake za kumuunga mkono rais William Ruto, hasa katika siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Ondiek amesema kuwa sababu kubwa ya rais William Ruto kupata uungwaji mkono kutoka kwa wakaazi wa Pwani, ni ukakamavu wa Aisha Jumwa katika kumpigia debe.
Aidha, Ondiek amekisia kuwepo kwa wanasiasa ambao wanatumia muungano wa wahandisi, katika kupinga uteuzi wa Aisha Jumwa.
Ikumbukwe kuwa hapo jana, Aisha Jumwa alikabidhiwa rasmi afisi hiyo ya mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini.

