IDARA YA USALAMA KAUNTI YA TANA RIVER YATAKIWA KUKABILIANA NA UTUMIZI WA MIHADARATI.

Idara ya usalama katika eneo bunge la Garseni kaunti ya Tana River imetakiwa kuweka sheria ya kudhibiti uuzaji na hata unywaji wa pombe kwenye mabaa eneo hilo.

Ni wito ambao umetolewa na mwenyekiti wa jamii ya Wardei eneo hilo Dahir Bille, ambaye amesema kuwa hatua ya ongezeko la sehemu za unywaji pombe, ndiyo chanzo cha vijana kuuwana kwenye jamii, baada yao kubugia pombe.

Dahir amesisitiza haja ya idara ya usalama, kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya ili kunusuru vijana wa eneo hilo, dhidi ya kupotoka kimaadili.

Wakati uo huo, amelalamikia ongezeko la idadi ya visa vya mauaji kati ya jamii za wafugaji kaunti hiyo, kwa kutimia visu.