Viongozi wa chama cha wiper kaunti ya Mombasa wameunga mkono kuidhinishwa kwa jopo la tume ya IEBC, litakalo endeleza mchakato wa kuwateua makamishna wa tume hiyo.
Wanachama hao wametetea suala la chama hicho kuchelewesha uteuzi wa makamishna wa tume ya IEBC, kutokana na hatua ya wao kuwasilisha kesi kuhusiana na uteuzi huo mahakamani.
Wakiongozwa na mwanaharakati na mshirikishi wa chama hicho kaunti ya Mombasa, Millicent Odhiambo ameishtumu serikali kwa kuendeleza siasa zinazo wahadaa wakenya, katika masuala mbali mbali ya taifa hili, ikiwemo uteuzi wa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Kwa upande wake aliyekuwa muwaniaji wa ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2022 eneo Changamwe, Munyoki Chalo amesisitiza kuendelezwa kwa shughuli za usajili wa wapiga kura, kama ilivyo anzishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya IEBC, Wafula Chebukati.

