Wazazi katika wadi ya Sabaki eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wamesisitizwa kuwapeleka wanao shuleni, muhula huu wa kwanza wa mwaka 2025.
Naibu chifu wa eneo la Msabaha Anne Ziro, amewataka wazazi wanaokabiliwa na changamoto zinazo changia suala la wao kutowapeleka wanao shuleni, kufahamisha idara ya usalama eneo hilo.
Anne amewashauri wazazi walio na watoto wanaoanza masomo ya chekechea, kuwapeleka katika shule zilizo karibu na makaazi yao.
Naibu chifu huyo aidha, amesema kuwa idara ya usalama katika eneo hilo kwa ushirikiano na wazee wa mtaa, itaanzisha msako dhidi ya wazazi watakao kosa kuwapeleka wanao shuleni wiki ijayo jumatatu.

