Baadhi ya wandani wa mwanasiasa Aisha Jumwa wamepongeza hatua ya rais William Ruto kumteua kiongozi huyo kuwa mwenyekiti wa bodi ya barabara humu nchini.
Wakiongozwa na Abdrahman Omar, wamemtaja Rais Ruto kuwa kiongozi ambaye anayejali wakaazi wa kaunti za Pwani kutokana na hatua yake kumteua Jumwa kwenye wadhifa huo.
Wakizungumza na wanahabari hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi, wameelezea kuwa na imani ya kuboreka kwa barabara za kaunti ya Kilifi na Pwani kwa jumla kutokana na uteuzi huo.
Aidha wameahidi kuendelea kuunga mkono serikali ya Kenya kwanza kwa madai kuwa inajali wananchi na viongozi wa Pwani.
Aidha Jumwa awali alibanduliwa kwenye baraza la mawaziri, alipokuwa akihudumu kama waziri wa jinsia.

