Wazazi kaunti ya Kilifi wametakiwa kushirikiana na walimu ili kuhakikisha kuwa wanao wanafanikiwa kwenye masuala ya elimu.
Ni wito ambao umetolewa na Mbunge wa Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi Owen Yaa Baya, ambaye amesema kuwa mafanikio ya wanafunzi hutegemea pakubwa jinsi ambavyo, wazazi huunga mkono utendakazi wa walimu shuleni.
Owen vile vile amewataka wazazi kufuatilia elimu ya wanao, kwani ni njia mojawapo ya kushurikiana na walimu katika kuboresha matokeo ya wanafunzi shuleni.
Naibu kinara huyo wa wengi kwenye bunge la kitaifa nchini, amepigia debe utendakazi wa serikali kuu huku akisema kuwa huenda tatizo la ukosefu wa walimu shuleni likapata suluhu la kudumu.

