WAZAZI KAUNTI YA TANA RIVER WATAKIWA KUHAKIKISHA WANAO WANAREJEA SHULENI MWAKA HUU 2025.

Wazazi eneo la Kilelengwani kule kaunti ya Tana River wametakiwa kuhakikisha kuwa wanao wanarejea shuleni kwa muhula wa kwanza mwaka huu wa 2025.

Akitoa wito huo chifu wa eneo hilo Jilo Mohameed Dhadho, amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwarudisha watoto wao maeneo ambayo wamekuwa wakisoma kwani wengi wao walisafiri maeneo ya mbali msimu wa likizo ndefu ya mwezi uliopita wa disemba.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Dhadho amewaonywa wazazi dhidi ya kuwaruhusu wanao kuendeleza shughuli za biashara ya maembe na ufugaji badala ya kuwasisitiza kurejea shuleni kuendeleza masomo.

Aidha Chifu Mohamed amesema kuwa wazazi wa watoto ambao watakosa kurejea shuleni watakabiliwa kwa mujibu wa sheria kwani watakuwa wamekiuka haki za mtoto.