Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ana wasiwasi timu yake “haiko tayari” kwa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham leo Ijumaa Agosti 16, 2024.
Ten Hag amehoji kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Matthijs de Ligt na Noussair Mazraoui watakuwa kwenye kikosi lakini waliwasili Alhamisi pekee. Wamekuwa na nafasi finyu ya kufanya mazoezi na wenzao wapya.
Wakati uo huo, beki Luke Shaw amekuwa nje ya uwanja kutokana na jeraha la mguu, mlinzi mpya wa £52m Leny Yoro yuko nje kwa miezi mitatu tangu mwanzoni mwa Agosti, na fowadi Rasmus Hojlund ana tatizo la misuli ya paja.
United ilijitolea kutumia karibu pauni milioni 60 kwa kuwaleta mabeki De Ligt na Mazraoui kwenye klabu kutoka Bayern Munich.
“Timu haiko tayari lakini ligi inaanza,” alisema Ten Hag.
“Kuna wakufunzi zaidi ambao wana shida hii lakini lazima tuanze.
“Hatuwezi kujificha kutoka kwake. Hatuwezi kuikimbia. Tunapaswa kukabiliana nayo.”
Man United inamenyana na Fulham katika uwanja wa Old Trafford kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu mpya 2024/25.
Upi ubashiri wako?

