MCHUNGAJI EZEKIEL ODERO AWASILISHA OMBI LA MAHAKAMA KUTOMZUIA KWA SIKU 30.

Mawakili wanaomuwakilisha mchungaji wa kanisa la new life prayer centre, Mavueni,Ezekiel Odero kaunti ndogo ya Kilifi kaskazini kaunti ya Kilifi wamewasilisha ombi kwenye mahakama ya Shanzu la kuzuilia mahakama dhidi ya kutoa uamuzi wa kutoachiliwa kwa mchungaji huyo.

Wakizungumza nje ya mahakama hiyo hii leo wakiongozwa na Danstan Omari, mawakili hao wametaka mahakama kuwasikiliza na kutokaidi ombi lao la kutaka Ezekiel awachiliwe pasipo kuzuiliwa kwa siku 30.

Aidha wamehoji kuwa wako tayari kukabiliana na upande wa mashtaka wakiamini kuwa mteja wao hana hatia na mashtaka dhidi yake ni ya uvumi tu.

Wakili Omari ametoa wito kwa wakaazi ambao wanaushahidi kwamba wapendwa wao walizikwa katika shamba la kanisa la new life prayer centre wajitokeze.