Ni afueni kwa waumini wa kanisa la Malindi Methodist mjini Malindi kaunti ya Kilifi baada kurejea katika kanisa lao lililokuwa limefungwa kwa miaka mitat kutokana na kile wanachodai kuchangiwa na uongozi mbaya wa dhehebu hilo nchini.
Wakiongozwa na Askofu wa dhehebu hilo ukanda huu wa Pwani, Gambo Davis Matano ametaja suala la waumini wa dhehebu hilo Pwani kupendekeza kubadilishwa kwa uongozi wa kanisa hilo nchini ndicho chanzo cha mizozo kuanza kushuhudiwa katika kanisa hilo mjini Malindi na hata Pwani.
Akizungumza na wanahabari amesema licha ya juhudi za idara ya usalama eneo la Malindi na kuanti ya Kilifi kutaka kutatua suala hilo bado juhudi hizo hazijafaulu.
Kwa upande wake mchungaji anayesimamaia kanisa hilo kwa sasa Ethel Mambo ameeleza kugadhabishwa na hatua ya kufungwa kwa kanisa hilo kwani wamegharamika zaidi katika kuliimarisha.
Kauli hiyo imeungwa mkono na mwenyekiti wa usimamizi wa kanisa hilo Patience Mchombo pamoja na waumini wengine ambao wameeleza kufurahishwa na hatua ya wao kuingia katika kanisa hilo na kuwataka waumini wenza kujitokeza na kuabudu pamoja nao na pia kuwataka kuendelea kudumisha amani.

