RAIS RUTO AMTAKA RAILA KUTUMIA KATIBA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAKENYA

Rais William Ruto amemtaka kinara wa Azimio Raila Odinga kutumia katiba kutatua changamoto zinazowakabili wakenya.
Rais amezungumza haya katika ikulu ya Nairobi alipomuapisha solisita mkuu mpya shadrack Mose ambapo amesema kuwa kila mkenya bila kujali cheo au tabaka anapaswa kutii sheria ya taifa kwa mujibu wa katiba.
Rais Ruto amesema kuwa kamwe hataruhusu watu wachache walio na sababu za kibinafsi kushiriki katika kuvunja sheria za katiba kwa kunyima wananchi wengine uhuru wao wa kutangamana na kufanya biashara akishutumu mrengo wa azimio kwa kutatiza uhuru wa wengine hasa katika maeneo ambayo yalishuhudia maandamano hapo jana.