MRADI WA SAN MARKO ULIOKO NGOMENI KAUNTI YA KILIFI KUBORESHA UHUSIANO MWEMA BAINA YA KENYA NA ITALIA

Serikali kuu imesema ipo haja ya wakenya kunufaika na mradi wa serikali ya Italia wa San Marko, ulioko katika eneo la Ngomeni eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Waziri wa ulinzi nchini Aden Duale, licha ya mradi huo kuboresha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, juhudi zaidi zinapaswa kuwekwa ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi, wanapewa mafunzo ya uhandisi na mawasiliano kupitia kituo hicho.
Akizungumza wakati alipozuru kituo hicho akiandamani na rais wa taifa la Italia Sergio Mattarella pamoja na Gavana wa kaunti ya Kilifi, waziri huyo amepongeza hatua ambazo taifa la Kenya limepigwa kiteknolojia hasa katika idara ya usalama, kutokana na kuimarika kwa shughuli hizo katika eneo hilo la San Marko.
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro amelalamikia hilo la Magarini na kaunti ya Kilifi kwa jumla, kusalia nyuma kimaendeleo licha ya taifa la Italia kuwekeza mradi mkubwa zaidi nchini katika kaunti ya Kilifi na kusema sharti watekeleze miradi ya maendeleo, ambayo itawafaidi wananchi katika eneo bunge hilo na kaunti ya Kilifi kwa jumla.