Taasisi ya utafiti wa kilimo na ufugaji KALRO imezindua aina mpya ya mbegu za Korosho ambazo zina uwezo wa kutoa mazao mengi ikilinganishwa na mbegu za kawaida.
Aina hizo nne ni pamoja na K-Korosho 75, 81, 82 na K-Korosho 100.
Kulingana na KALRO, mbegu hizi mpya zina uwezo wa kustahimili kiangazi na pia mmea wake unaanza kutoa mazao yake mapema, mwaka mmoja na nusu baada ya upanzi.
Wakulima katika katika kaunti nne za pwani, Kwale, Kilifi, Lamu na Tana River wataanza kununua miche kwa Sh.100 kwa ajili ya upanzi katika mashamba yao.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja wa KALRO mjini Mtwapa na kuongozwa na katibu katika wizara ya Kilimo nchini Kello Harsama pamoja na Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy.

