GAVANA ABDULSWAMAD ASEMA HAWATARUHUSU KUBINAFSISHWA KWA BANDARI YA MOMBASA

Mikakati inapoendelezwa na serikali kuu kuboresha bandari zilizoko nchini Kenya, Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amepinga hatua ya kutaka kubinafsishwa kwa bandari ya Mombasa.
Kauli ya gavana Nassir inajiri baada ya kuibuka tetesi kuna baadhi ya watu wanaopanga kuibinafsishwa kwa bandari hiyo ya Mombasa ambayo ni tegemeo kuu kwa wenyeji wa pwani.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa kwenye mkutano uliowaleta pamoja viongozi mbalimbali wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Nassir amesema hawataruhusu hilo kufanyika.
Katika suala la kupanda kwa gharama ya Maisha gavana Nassir amewataka viongozi walioko mamlakani nchini kushirikiana na kuliangazia suala hilo ili kuwanusuru Wakenya ambao wanaendelea kuathirika na gharama ya Maisha.