AFISI YA MBUNGE WA MALINDI IMEELEZA KUWEPO KWA MIKAKATI YA KUJENGA SHULE ZA UPILI KATIKA KILA SHULE YA MSINGI

Afisi ya mbunge wa Malindi kaunti ya KIlifi, Amina Mnyazi imeeleza kuwepo kwa mikakati ya kujenga shule za upili, katika kila shule ya msingi iliyoko eneo bunge la Malindi.
Kulingana na mratibu wa mipango katika afisi hiyo Dickson Chilango, hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuboresha masomo ya wanafunzi katika eneo la Malindi, kwani kumekuwa na idadi ndogo ya shule za upili eneo bunge la Malindi.
Chilango amesema hatua hiyo itawasadia wanafunzi waliomaliza darasa la nane katika eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, kujiunga na shule za upili na kuendeleza masomo yao, suala ambalo litasadia kutekeleza agizo la serikali kuu la kuwataka wanafunzi kujiunga na shule za upili kwa asilimia mia moja.
Aidha, ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu katika eneo bunge la Malindi kujitokeza na kushirikiana na uongozi wa eneo la Malindi ili kufanikisha suala hilo ambalo pia litapunguza idadi ya wanafunzi katika shule zilizo na wanafunzi wengi zaidi, ikilinganishwa na rasilimali zilizoko katika taasisi hizo kwa sasa.