Naibu kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Tana River Hamid Babusa na mwakilishi wa wadi mteule Lucy Diramo wameitaka serikali kuu kukataa misaada kutoka kwa mataifa ya nje au mashirika ambazo zinakuja na masharti ya kukubali mapenzi ya Jinsia moja.
Kauli zao zinajiri baada ya bunge la kaunti ya Tana River kupitisha hoja ya kuitaka serikali kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu au mashirika ambayo yanaunga mkono mapenzi ya jinsia moja.
Wamesema taifa la Kenya lina raslimali nyingi ambazo zinaweza kuboresha nchi bila kutegemea misaada hiyo.
BAADHI YA VIONGOZI WA KAUNTI YA TANA RIVER WAITAKA SERIKALI KUU KUKATAA MISAADA KUTOKA MATAIFA YA NJE

