WADAU MBALI MBALI ENEO LA MALINDI KAUNTI YA KILIFI WASHIRIKIANA KATIKA ZOEZI LA UPANZI WA MITI.

Kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia inchi katika eneo hili la Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla, wadau mbali mbali wa kimazingira kaunti ya Kilifi, wameendeleza shughuli za upanzi na utunzi wa miti katika bustani ya Buthwani water front Park.

Kulingana na mwanzilishi wa mpango wa upanzi wa miti milioni moja Elphic Tossi, ni kuwa wale wanaojihusisha na upanzi wa miti hiyo katika bustani hilo, pia wanapewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanatunza miti yao kwani watatuzwa iwapo miti waliyopanda itasawi vyema.

Akizungumza na lulu fm, amesema kuwa hatua hiyo pia itaboresha mazingira ya kituo hicho katika siku za osoni na hata kusaidia wale watakao kuwa wakitembelea sehemu hiyo ili kupata kivuli.

Aidha, ametoa wito kwa wahisani kujitokeza na kuwasaidia katika kuafikia malengo yao ya kupanda miti milioni moja kaunti ya Kilifi, ikiwa ni pamoja na kuwachimbia kisima kitakacho wasaidia katika kunyunyizia maji miche inayoendelea kupandwa katika eneo hilo.