Naibu kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Christine Kilalo amewahimiza wanawake katika kaunti hiyo kuwania nafasi mbalimbali za uongozi baada ya kubainika ni asilimia 5 pekee ya wanawake ambao walichaguliwa kwenye kipute cha uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka jana wa 2022.
Kilalo amesema kutokana na hilo sasa wameanzisha harakati za kuwahimiza wanawake wengi kujitokeza katika kuwania nyadhifa za uongozi.
Vilevile, amesema wanashinikiza usawa kwa wanawake ambao wako kwenye bunge la kaunti ya Taita Taveta.
WANAWAKE KAUNTI YA TAITA TAVETA WAHIMIZWA KUWANIA NAFASI ZA MBALIMBALI ZA UONGOZI

