SERIKALI YA KAUNTI YA LAMU KUWAFADHILI KIMASOMO WANAFUNZI WANAOTOKA MAENEO YA BASUBA

Naibu Kamishna wa kaunti ya Lamu Raphael Munyua amesema wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia zisizojiweza na ambao wanapata zaidi ya alama ya 250 kwenye mtihani wao wa darasa la 8 KCPE watafadhiliwa masomo yao ya upili na serikali ya kaunti ya Lamu ili kuendeleza masomo yao.
Kulingana na Munyua, wanafunzi kutoka maeneo ya Basuba ambao wanaishi kwenye Msitu wa Boni ambao unaaminika kuwa ngome ya magaidi wa Al –Shabaab wanasomea katika mazingira magumu.
Ameitaja kama hatua ambayo inapania kuinua viwango vya elimu katika maeneo hayo yaliyosahaulika ambapo kuna idadi ndogo ya wanafunzi ambao walimaliza masomo yao ya shule za upili.

Serikali ya kaunti ya Lamu inawafadhili wanafunzi wote wanaopata alama ya 300 kwenye mtihani wa darasa la 8 ila kwa wanafunzi hao kutoka Basuba wamewekewa alama ya 250.