Bodi inayaoangazia marupurupu ya wafanyakazi wa serikali nchini ya PUBLIC SERVICE SUPERANNUATION SCHEME, iwamehakikishia wafanyakazi wa serikali kutocheleweshwa kwa pesa zao za uzeeni baada ya kustaafu.
Akizungumza mjini Malindi kaunti ya Kilifi, katika kikao cha kuhamasisha wafanyakazi wa serikali kuhusiana na pesa za uzeeni, afisa wa bodi hiyo Douglas Asanya, amesema afisi ya msimamzi wa wafanyakazi wa umma, tayari ilitoa mwelekeo mpya kuwa wale wanaostaafu, watapokea barua ya kuwataka kuanza kutayarisha stakabadhi hitajika mwaka mmoja kabla ya wao kusataafu ili kupata fedha zao kwa wakati.
Kwa upande wake Annah Kitole mmoja wa maafisa anayehusiaka na malipo ya uzeeni, amesema tayari wameweka maafisa wa bodi ya malipo ya uzeeni, katika afisi mbalimbali za wafanyakazi wa umma kama vile ya walimu na polisi ili kurahisisha shughuli za wafanyakazi wao kupata pesa za uzeeni bila changamoto zozote.
Aidha, baadhi ya waliohudhuria kikao hicho cha kupokea hamasa hizo wakiongozwa na naibu kamishna wa eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Peter Thiong’o wamesema wafanyakazi wa serikali wamekuwa wakichangia pakubwa katika kuchelewa kwa malipo yao ya uzeeni, kutokana na hatua ya wao kukosa kufuata taratibu hitajika.
WAFANYIKAZI WA SERIKALI KUPOKEA FEDHA ZAO ZA UZEENI KWA WAKATI

