AHMED KOMBO AHMED AELEZA KURIDHISHWA NA HATUA ZIMEPIGWA KUFANIKISHA MTAALA WA CBC

Naibu katibu wa muungano wa walimu KNUT tawi la Mombasa Ahmed Kombo Ahmed ameeleza kuridhishwa na hatua na mikakati iliyoko katika utekelezaji wa mtaala wa umilisi wa CBC hadi kufikia sasa tangu kuanzishwa nchini.
Akizungumza na wanahabari Kombo amesema wazazi wanapaswa kuthamini mtaala huo na pia kujukumika katika kuwatimizia mahitaji mbalimbali ya watoto wao ili kuendeleza masomo yao vyema.
Amewataka wazazi kuwanunulia watoto wao sare za shule kulingana na kanuni za wizara ya elimu nchini na kuwahimiza wazazi pamoja na kamati ya shule kujadiliana na kuelewana namna wanafunzi watakuwa wakila chakula shuleni ili kudhibiti njaa kuwakabili…….
Aidha, Kombo amesema tume ya kuajiri walimu TSC imeanza kuwatuma walimu kwenye shule mbalimbali nchini ili kuufanikisha vyema mtaala wa CBC kama ulivyokuwa umepaniwa.