Wito umetolewa Kwa wazazi wote katika kaunti ya Taita Taveta hususan walio na watoto wanaojiunga na gredi ya Saba Kwa masomo ya sekondari msingi kuwapeleka shuleni.
Haya ni Kwa mjibu wa mwenyeketi wa muungano wa wazazi Kaunti ya Taita Taveta Elius Mberi ambaye amesistiza Kuwa masomo hayo ni bure na kila mtoto nchini anapaswa kuhudhuria masomo kwani ni haki yao kikatiba.
Amesema kuna baadhi ya wazazi ambao wameanza kuibua sababu mbalimbali zisizokuwa za kimsingi hali ambayo inasababisha watoto wao kutojiunga na gredi hiyo ya saba.
Haya yanajiri huku idadi kubwa ya wazazi Kaunti ya Taita Taveta wakilalamikia kulipishwa ada ya usajili kwa watoto wao kama mojawapo ya masharti kabla ya kuruhusiwa kujiunga na Gredi ya 7.
Hii ni hata baada ya serikali kupitia waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu kuamuru walimu wakuu wa shule za msingi kutowatoza wazazi ada yoyote, wakati wa zoezi la kuwasajil wanafunzi hao wa masomo ya sekondari msingi, linaloendelea kote nchini.
WAZAZI KAUNTI YA TAITA TAVETA WAHIMIZWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULENI

