Jamii ya Wapemba inayoishi kaunti ya Kwale imempongeza rais William Samoei Ruto kwa kuidhinisha rasmi uraia wao wa Kenya kupitia gazeti rasmi la serikali.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Hamisi Makame, jamii hiyo ambayo imekuwa ikiishi nchini kwa miaka mingi imeeleza kufurahishwa na agizo la rais la kutaka jamii hiyo itambuliwe kuwa miongoni mwa makabila ya Kenya.
Jamii hiyo imesema sasa itapata fursa ya kumiliki ardhi baada ya kupata vitambulisho vya kitaifa kutoka kwa serikali………
Aidha, jamii hiyo imedai kunyimwa fedha za mikopo na kukosa akaunti za benki kufuatia ukosefu wa stakabadhi hiyo muhimu na kuhangaishwa na maafisa wa polisi hasa wanapoendeleza shughuli zao za uvuvi baharini.
Haya yanajiri baada ya jamii ya Wamakonde inayoishi pia kaunti hiyo kupatiwa uraia wa Kenya na serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

