Serikali ya kaunti ya Kwale imeanzisha ugavi wa chakula cha msaada kwa watu wenye uatilifu, wajane na mayatima.
Ni hatua ambayo inajiri wakati ambapo baa la njaa linaendelea kuwakabili takribani wenyeji laki 2 katika kaunti ya Kwale kutokana na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu.
Mwakilishi wa kike kaunti ya Kwale Fatuma Masito na mshirikishi wa idara ya Jinsia Nelly Amoite wamesema msaada huo unalenga kuhakikisha wanafunzi wanaendeleza masomo yao bila changamoto zozote zinazosababisha na njaa.
UGAVI WA CHAKULA CHA MSAADA WAANZISHWA NA SERIKALI YA KAUNTI YA KWALE

