NAIBU GAVANA WA LAMU AMEWAHAKIKISHIA WENYEJI WA MARARANI HUDUMA BORA ZA MAJI

Naibu Gavana wa kaunti ya Lamu Rapahel Munyua amewahakikishi wenyeji wa Mararani eneo bunge la Lamu Mashariki huduma bora za maji kutoka katika serikali ya kaunti ya Lamu.
Akizungumza katika eneo hilo la Mararani amesema serikali itaanzisha zoezi la ugavi wa dawa za kuyasafisha maji wanayoyatumia wenyeji ili kudhibiti magonjwa mbalimbali yanayotokana na maji chafu.
Amesema lengo la serikali ya kaunti ya Lamu ni kuhakikisha wenyeji wote wa kaunti ya Lamu wanahudumiwa ipasavyo.