Mwenyekiti wa Msalaba mwekundu kaunti ya Mombasa Mahmoud Noor amesema zaidi ya vijana 450 wamefaidika kutokana na mafunzo ya namna ya kutafuta ajira kupitia mashirika ambayo siyo ya kiserikali.
Mahmoud amesema mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na shirika la Msalaba Mwekundu katika kaunti hiyo yalijumuisha vijana kutoka maeneo bunge yote 6 ya Mombasa.
Amesema kupitia mafunzo hayo vijana hao wamefanikiwa kujifunza mambo mengi kama afya ya akili pamoja na kujiendeleza kibiashara miongoni mwa mengine.
ZAIDI YA VIJANA 450 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA NAMNA YA KUTAFUTA AJIRA KAUNTI YA MOMBASA

