Baadhi ya viongozi wa kijamii kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa wabunge pamoja na wanasiasa wote, kutekeleza haki na usawa katika zoezi la ugavi wa fedha za basari kwa wanafunzi wote.
Kwa mujibu wa kiongozi wa muungano wa wazee wa kimijikenda wa Malindi District Cultural Association, Stanely Kiraga , ugavi wa basari haupaswi kuzingatia masuala ya siasa, kwani ni haki ya kila mtoto anayetoka katika familia isiyojiweza kifedha kunufaika na fedha hizo.
Akizungumza na lulu Fm Kiraga amesema iwapo hilo litazingatiwa watoto wanaotoka kwenye familia zisizojiweza kifedha zitanufaika na kuweza kendeleza masomo yao bila changamoto zozote.
Aidha, amewataka wawakilishi wa wadi kuwa na idadi kamili ya wanafunzi wanalio na uhitaji wa karo katika maeneo yao, ili kuhakikisha wanapeta fedha hizo za basari kutoka kwa hazina ya maeneo bunge ya CDF.
HIMIZO LATOLEWA KWA VIONGOZI WOTE KUHAKIKISHA MGAO WA BASARI UNAWALENGA WALIO NA UHITAJI

