Idadi ya watalii wanaozuru taifa la Kenya inaendelea kuongezeka.
Hii n baada ya meli yenye watalii 620 kutoka mataifa ya nje kutia nanga katika bandari ya Mombasa.
Meli hiyo imepokelewa na katibu katika wizara ya utalii nchini John Olultuaa ambaye amesema hiyo ni meli ya tatu kuwasili ikiwa na watalii baada ya meli ya kwanza kuwasili mwezi Novemba na ya pili mwezi Disemba mwaka jana wa 2022.
Olultuaa amesema ujio wa watalii hao kutachangia katika kuimarisha sekta ya utalii nchini..
Aidha, amesema watalii hao watazuru sehemu mbalimbali za kitalii pamoja na mbuga za wanyama kanda ya pwani na maeneo mengine nchini.
Vilevile, amesema mikakati thabiti imewekwa na wizara ya utalii nchini kwa ushirikiano na asasi zingine za serikali ili kuimarisha sekta hiyo, kauli ambayo imeungwa mkono na kaimu mkurugenzi wa utalii John Chirchir ambaye amesema wanatarajia watalii zaidi kuwasili nchini .
WATALII ZAIDI WANATARAJIWA KUZURU KENYA

