BAADHI YA WAKAZI WA KILIFI MJINI WASEMA MTAALA WA CBC ULIPASWA KUPIGWA MSASA KABLA YA KUTEKELEZWA

Baadhi ya wazazi Kilifi Mjini kaunti ya Kilifi  wamelalamika kuwa mtaala wa umilisi wa CBC bado ulipaswa kuangaziwa kwa kina kabla ya kutekelezwa.

Wazazi hao wamesema kuwa serikali haijajipanga kufanikisha mtaala huu hasa katika shule za mashinani kwani bado zina miundo msingi duni.

Kufuatia hilo wazazi hao wanahofia kuwa huenda kukawa na wingi wa changamoto katika kutekeleza mchakato mzima wa cbc kwenye shule hizo.

Aidha wanasema pia sera kamili ya mtaala wa elimu pia haijawekwa wazi wakati tayari shule zikiwa zimefunguliwa.