Mwakilishi wa wadi ya kipevu kaunti ya Mombasa Leila Nyache ameshirikiana na machifu, wazee wa mitaa na mabalozi wa nyumba kumi kwenye zoezi la upanzi wa miti ndani ya shamba la AKAMBA HANDCRAFT eneo bunge la changamwe kaunti hiyo ya Mombasa.
Akiongea na wanahabari wakati wa zoezi hilo leila amesema wanapania kupanda miti mia tano na tayari wamemudu kupanda miti 300 akiamini kuwa wanaweza kuafikia malengo hayo kwa wakati ufaao.
Hata hivyo Leila amesema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu huku akihimiza jamii kupanda miti ili kuhifadhi na kuweka mazingira bora.

