VIJANA WENGI KAUNTI YA TAITA TAVETA HUSUSIA KUJIUNGA NA TAASISI ZA ELIMU ZILIZOKO KWENYE KAUNTI HIYO

Mbunge wa Voi kaunti ya Taita Taveta Abdi Chome amesema wamebaini sababu zinazosababisha vijana wengi kususia kujiunga na taasisi za elimu zilizo katika kaunti hiyo.

Chome amesema sababu mojawapo ni kwamba vijana wengi wanapania kujiunga na vyuo vya nje ya kaunti hiyo kutokana na swala kuwa masomo yao ya shule za msingi na sekondari walikuwa kwenye shule za kaunti hiyo.

Mbunge huyo pia amesema vijana wengine pia hushindwa kufikisha alama hitajika kujiunga na taasisi hizo huku akisema kuwa sababu hizo zimechangia uhaba wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Taita Taveta.